Luke 1:46-55

Wimbo Wa Maria Wa Sifa

46 aNaye Maria akasema:

“Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47 bnayo roho yangu inamfurahia
Mungu Mwokozi wangu,
48 ckwa kuwa ameangalia kwa fadhili
unyonge wa mtumishi wake.
Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,
49 dkwa maana yeye Mwenye Nguvu
amenitendea mambo ya ajabu:
jina lake ni takatifu.
50 eRehema zake huwaendea wale wamchao,
kutoka kizazi hadi kizazi.
51 fKwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake;
amewatawanya wale wenye kiburi
ndani ya mioyo yao.
52 gAmewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi,
lakini amewainua wanyenyekevu.
53 hAmewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri,
bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54 iAmemsaidia mtumishi wake Israeli,
kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu
55 jAbrahamu na uzao wake milele,
kama alivyowaahidi baba zetu.”
Copyright information for SwhNEN